Kugeuza maandiko matakatifu kwa lugha

Kazi za kugeuza maandiko matakatifu na jamaa kubwa ya CITBA, pamoja na usiano ya makanisa iliounda kundi na pia wageni ambao wanatusaidia ndani ya kazi sawa SIL-ECG, CITBA inaunda mipango ya kuanjisha kazi ya kugeuza Biblia kwa luga ya Jimbo. Kwa sasa tuna lugha sita ambao kazi inafanyika yani Budu, Lika, Komo, Mangbetu, Mayogo et Logo. Wengine sawa Mayogo na Logo wamemaliza kazi ya Agano Jipia na wengine wanasonga na kazi.

CITBA ni kundi ilioundwa kwa usiano ya makanisa. Makanisa inachagua na kuleta watu ambao wanastahili kisha kufundishwa kazi wafanye kazi ambao ina matokeo mema na kukubaliana na watu wa luga (traduction exacte, claire, naturelle, et adaptée). Katika picha ifatayo mutaona kiongozi ya kazi ya utafsiri na watafsiri Anzalekyeho Abati François, na pia wengine ambao wanatayarishwa kuwa wachunguzaji ya kazi ya utafsiri.

Ndani ya luga sita ambao inatumika ndani ya CITBA mbili imemaliza kazi ya Agano Jipia ku mwaka 2016 mwezi wa tatu (Mayogo na Logo). Kwa wengine kazi inasonga mbele. CITBA ina piga kilio kwa ajili wa lugha zote za jimbo wapate neno la Mungu kwa lugha zao. Itakuwa furaha kubwa wakati watu wa kila luga watakuwa na Neno la Mungu kwa lugha zao. 

translators.jpg
Share

Your encouragement is valuable to us

Your stories help make websites like this possible.