Kujionesha

Kundi la usiano ya makanisa kwa ajili ya ugeuzi na kusomesha Bibilia kwa lugha yaani CITBA ni kundi isiousika na mambo ya pesa, ni kundi ya kiKristu kwa ajili ya kusaidia makanisa ambayo iliunda kundi lile ; kwa ngambo ya Katolika kuna jimbo tatu (Diocèses) yaani Isiro-Niangara, Dungu-Doruma pia Wamba; kwa ngambo ya kiprotestati tuna ECC/ 12ème AOG, 16ème CECCA tena 20ème CECA. CITBA ina usiano ya kazi na SIL-ECG, SEED COMPANY pia makanisa iliounda kundi ya CITBA. Pia ina vibarura ya serekari inayomuruhusu kufanya kazi katika jimbo letu.

CITBA inapatikana ISIRO, muji mukuu wa jimbo la Haut-Uele, Kaskazini-Mashariki ya Congo RD. Tunafanya kazi ndani ya nyumba mbili zenye makanisa ilitolea kwa ajili ya kazi, yaani Adminisatration ndani ya ville ya Isiro pembeni ya shule ya juu ya Uele (Université de l’Uélé), pia Chumba ya kugeuza Bibilia kwa lugha inapatikana ku Mukoba AGBIANO namba 3.

Share

Your encouragement is valuable to us

Your stories help make websites like this possible.